Thursday, 8 May 2014

Listi ya vilabu vyenye utajiri duniani: Man Utd, Real Madrid, FC Barcelona nani kashika nafasi ya kwanza?


forbesmost-valuble-soccer-teamsKlabu ya Manchester United imezidi kushuka chini kwenye chati ya vilabu vyenye thamani kubwa ulimwenguni, kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Nafasi ya kwanza imeshikwa na klabu ya Real Madrid yenye thamani ya £2billion, nafasi ya pili FC Barcelona ambayo imetajwa kuwa na thamani ya £1.9billion.
United baada ya kuwa msimu mbaya kabisa kwenye historia yao, wameshuka kutoka nafasi ya 2 mwaka jana mpaka nafasi ya 3 wakiwa na thamani ya £1.65billion.
Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wameshika nafasi ya nne kwa kuwa na thamani ya £1.1billion, wakati huo huo klabu ya Manchester City imeweza kupanda thamani kwa asilimia 25 wakiwa na thamani ya  £508m.
LISTI KAMILI ILIVYO
984068_237972503058041_3057865779243803531_n

Taarifa kuhusu Kocha wa Yanga kusitisha mkataba wake na Yanga.



kochaTaarifa ambayo inatolewa muda huu na Uongozi wa Yanga ni juu ya kuacha kazi kocha wa timu hiyo Hans Van Der Plujim ambaye aliungana na timu hiyo January 2014,sababu za kocha huyo kuacha kazi ni kile kilichoelezwa kuwa amepata dili nchi nyingine na mkataba wake na Yanga ulikua unamalizika July mwaka huu.
Timu ambayo anaenda kocha huyo ipo nchini Saudi Arabia,

Thursday, 26 December 2013

TAMASHA LA KRISIMASI LAFANA UWANJA WA TAIFA,SOLLY MAHLANGU WA AFRIKA KUSINI AWAKUNA VILIVYO WATAZAMAJI



 Mgeni rasmi wa tamasha la Krisismasi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge,Mh.William Lukuvi akizungumza mbele ya watazamaji waliofika kwenye tamasha hilo jioni ya leo,lililofanyika ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar.Lukuvi amewataka watazamaji na washabiki wa tamasha hilo  na Watanzania kwa ujumla kusherehekea sikukuu ya krismasi na mwaka mpya kwa amani,upendo na utulivu,ameongeza kuwa pia Serikali itahakikisha usalama upo na wa kutosha kwa watu wake,pichani kati ni Mbunge wa Msalala,Mh.Ezekiel Maige pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions Ltd,ambao ndio waandaji wa tamasha hilo Bwa.Alex Msama.
 Mmoja wa wageni waalikwa katika tamasha la Krisimasi,Mbunge wa Msalala,Mh.Ezekiel Maige pichani kati akiwatakia heri na fanaka Watazamaji na Watazania kwa ujumla katika kusherehekea sikukuu ya Krisimasi na mwaka mpya. 
 Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka nchini Zambia,Epraim Sekereti akiimba jukwaani kwenye tamasha la krismasi jioni ya leo ndani ya uwanja wa Taifa,ambapo mgeni rasmi alikuwa Mh.Lukuvi.
  Baadhi ya Waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka kikundi cha Living Waters wakitumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Krisimasi lililofanyika jioni ya leo ndani ya uwanja wa Taifa,jijini dar.
 Baadhi ya waimbaji waliombatana na mwanamuziki nyota kutoka nchini Afrika Kusini Solly Mahlangu,wakimpa back up mkali huyo wa injili. 
 Baadhi ya Wapiga vyombo wa mwanamuziki Solly Mahlangu wakiwajibika jukwaani.
 Baadhi ya mashabiki wa Mwanamuziki Solly Mahlangu kutoka nchini Afrika kusini wakifurahia
 Pichani juu na chini ni Mwanamuziki mahiri kutoka nchini Afrika Kusini,Solly Mahlangu akiwaimbisha mashabiki wake jioni ya leo kwenye tamasha la krisimasi,lililofanyika ndani ya uwanja wa Taifa jijini dar. 
Sehemu ya umati wa watu waliofika kwenye tamasha hilo jioni ya leo.
 Mwimbaji wa nyimbo za Kiroho a.k.a Injili Upendo Nkone akiimba kwa hisia jukwaani jioni ya leo mbele ya mashabiki kibao (hawapo pichani) wakati wa tamasha la krisimasi likiendelea jioni ya leo ndani ya uwanja wa Taifa,jijini Dar.
 Pichani shoto ni Mwimbaji nyota wa muziki wa injili,Rose Muhando akiwa sambamba na skwadi lake zima,wakishambulia kwa namna ya pekee kabisa,huku miluzi na shangwe za watazamaji zikivuma kila kona ya uwanja,jioni ya leo kwenye tamasha la krisimasi.
 Rose Muhando akiimba wimbo wake wa Utamu kwa Yesu mbele ya mashabiki wake (hawapo pichani) jioni ya leo ndani ya uwanja wa Taifa,ambako tamasha la Krisimasi likiendelea jioni ya leo. 
 Muimbaji wa nyimbo za kuabudu,Upendo Kilahiro akiimba kwa hisia jukwaani jioni ya leo kwenye tamasha la krisimasi,linaloendelea hivi sasa ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar.

 Baadi ya Waimbaji wa kundi la Glorious wakiimba jukwaani 
Mwimbaji wa nyimbo za injili,Boni Mwaitege pichani kati na madansa wake wakiwaimbisha mashabiki wao jioni ya leo .
 Sehemu ya umati wa Watu wakifuatilia tamasha la Krisimasi,linalofanyika jioni ya leo ndani ya Uwanja wa Taifa,ambalo limejumuisha wanamuziki mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.
 Kundi la waimbaji mahiri wa muziki wa injili The Voice wakiimba Acapera zao jukwaani jioni ya leo kwenye tamasha la Krisimasi linalofanyika hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar.Tamasha hilo huandaliwa kila mwaka na kampuni ya Msama Promotions Ltd
 Mgeni rasmi wa tamasha la Krisismasi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu na Bunge,Mh.William Lukuvi akiwasalimia mashabiki watazamaji mbalimbali waliofika kwenye tamasha hilo,linalofanyika hivi sasa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar .

 

Diamond kamtangaza tena Wema



sddHii ilikuwa jana pale Leaders club kwenye show ya Diamond ambapo Wema Sepetu alipanda kwenye stage na kuongea na mashabiki waliofika kwenye show hiyo.
Kwenye hiyo show Diamond aliuliza,”Mnataka kumjua mchumba wangu”?
Show ilivyoendelea Diamond alitaka kuimba wimbo wa ukimwona akasema, “Naskia ninayetaka kumuimbia wimbo huu yupo humuhumu ndani”.
Wema Sepetu akapanda kwenye stage wakaimba na kucheza wote.
994992_654719497904805_1370630389_n
379719_654725334570888_100223854_n
1499625_654740321236056_1133727884_n


Saturday, 14 December 2013

WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO KUZINDUWA TAMASHA LA VIPAJI


Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kutoka kushoto ni Mwakilishi kutoka kampuni ya Zantel, Divine Mosi na Fadhil Nandonde kutoka UCA-Tz, kulia ni mwakilishi wa vijana kutoka nchini Uganda, Ms. Faridah Nalunkuma.Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kutoka kushoto ni Mwakilishi kutoka kampuni ya Zantel, Divine Mosi na Fadhil Nandonde kutoka UCA-Tz, kulia ni mwakilishi wa vijana kutoka nchini Uganda, Ms. Faridah Nalunkuma.Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa vijana kutoka nchini Uganda, Ms. Faridah Nalunkuma akizungumza na waandishi wa habari juu ya uwakilishi wake wa UCA, na kuzungumzia tamasha kwa ujumla.Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy alipozungumza nao juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA THEHABARI.COMBaadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya ukuzaji vipaji vya sanaa na muziki (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz), Emmanuel Mushy alipozungumza nao juu ya tamasha la UCA-Tz litakalofanyika kesho jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA THEHABARI.COM


KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa tamasha la vipaji vya sanaa na muziki lililoandaliwa na asasi ya ukuzaji vipaji (Unscripted Concert for Africa-Tanzania, UCA-Tz). 
Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa asasi hiyo, Emmanuel Mushy alisema tamasha hilo la pekee litakalofanyika Uwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam linatarajia kushirikisha vijana zaidi ya 500 kutoka maeneo anuai ya jiji. 
 Akifafanua zaidi juu ya tamasha hilo, Mushy alisema UCA-Tz ni program yenye dhumuni la kutoa nafasi kwa vijana wenye vipaji vya muziki na sanaa ili vijana hao waweze kukua katika vipaji vyao. “…Neno ‘unscripted’ linamaanisha kitu ambacho kipo lakini hakijaandikwa, yaani kwa maana nyingine ni kitu kilichopo nyuma ya pazia.
 UCA-Tz baada ya utafiti imebaini kuwa kuna vijana wengi ambao wanajihusisha na muziki pamoja na sanaa lakini hawapati ile nafasi (platform) ya kuendeleza vipaji vyao, hivyo ni kama vijana hawa wapo nyuma ya pazia,” alisema Mushy. 
 Aliongeza kuwa UCA Tz kwa kutambua umuhimu wa vipaji vya vijana vinavyopotea imeona umuhimu wa kutengeneza njia kwa vipaji hivyo ili vitoke nyuma ya pazia kukua na hatimaye kujionesha kwa jamii. Aidha alisema moja ya njia ambazo UCA-Tz inazifanya ni kuandaa matamasha ya vipaji kwa kila mwaka kuwashirikisha vijana na kwa mara ya kwanza inazindua Tamasha la vipaji nchini Tanzania, ambalo litashirikiza vijana zaidi 500 kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. 
 “…Tamasha hili la vipaji linatarajia kufanyika kesho, Jumamosi ya tarehe 14th December pale Uwanja wa Kinondoni Biafra, kuanzia saa 7 mchana hadi saa 12 za jioni. Katika tamasha hilo vijana wenye vipaji vya kuimba, ku-rap, kucheza, kuchora na ubunifu (ku-design) watawasilisha kazi zao kwa umati utakao jitokeza na vijana wenzao,” alisema Mushy. 
 Alisema ili kuleta radha na hamasa zaidi asasi hiyo imealika wawakilishi vijana kutoka nchi mbalimbali za Africa kama Kenya, Uganda na Ghana ambao nao watashiriki. “…Kutakua na outside performances kutoka kwa wasanii mbalimbali ambao wameshapiga hatua kwenye tasnia za muziki na sanaa nao watashiriki kwa pamoja. 
 Naye Mwakilishi kutoka kampuni ya Zantel, Divine Mosi ambao ni moja wa makampuni yaliofanikisha tamasha hilo, akizungumza alisema kampuni yao itaendelea kuunga mkono shughuli anuai za kuwawezesha vijana ikiwa ni sehemu ya kurudisha mchango wa wateja wao wanaotumia mtandao wao. 
 Kampuni nyingine zilizounga mkono kiushirikiano (supporters/sponsers) kufanikisha tamasha hilo ni pamoja na kampuni ya Coca Cola, Maezeki, Arise Media, LGBY Media na mtandao wa kijamii wa habari-Thehabari.com (www.thehabari.com) na mitandao mingine ya kijamii nchini.

   

MCHEZAJI WA ZAMANI WA KLABU YA MANCHESTER UNITED ANDY COLE ATUA JIJINI DAR


Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (kulia) akimkaribisha Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (kushoto) mara tu baada ya kuwasili nchini kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania . Kati kati ni Afisa Uhusiano wa klabu ya Manchester James Turner.
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole akikabidhiwa maua mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana usiku kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania .
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (kushoto) akimuongoza Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (katikati) kuelekea sehemu ya VIP kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)mara tu baada ya kuwasili nchini jana usiku.
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (kushoto) pamoja na Afisa Uhusiano wa klabu ya Manchester James Turner (kulia) wakikamilisha taratibu zakupata hati ya kuingia nchini kwenye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana usiku mara tu baada ya kuwasili kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania .
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (kulia) akimuelekeza jambo Afisa Uhusiano wa klabu ya Manchester James Turner (katika) mara tu baada ya kuwasili kwa mwaaliko wa kampuni ya Mawasiliano ya Airtel Tanzania . Kushoto ni Picha na Mpiga picha wetu. Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole.
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United Andy Cole (mbele) akitoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwelekea hotelini alipofikia mara bada ya kuwasili nchini jana usiku. Nyuma yake ni mwenyeji waka ambaye ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando . 


Friday, 22 November 2013

Pichaz zikionyesha video ya Diamond ikichezwaTRACE TV ya Ufaransa na Nigeria




d4Ni kituo cha TV miongoni mwa vituo vya TV vikubwa ambavyo huwa ni mara chache sana kutoa nafasi kwa video za Wasanii wa Afrika tena hasahasa Afrika Mashariki manake Wanigeria kwao sio tabu, wamekua na uwezo wa kutengeneza video nzuri ndio maana zao zinachezwa nyingi tu.
Baada ya video ya Diamond kuonekana usiku wa November 21 2013 huku TRACE TV wakiitambulisha kama video mpya, Platnums anakua msanii mwingine wa Tanzania baada ya Ay ambae ndio msanii wa kwanza video zake kuchezwa TRACE TV.
Pamoja na kuonyeshwa TRACE TV, video hii ya ‘number one’ imeonyeshwa pia kwenye kituo maarufu cha muziki Nigeria kiitwacho Sound City.
d3
d6
d3
d2
d1
d5

pengine huo waweza kuwa mwanzo wa diamond kujulikana kimataifa nani anajua?

Saturday, 9 November 2013

Kutana na tweet 14 za Mchekeshaji Mpoki



0
Kutana na tweets za mkali wa comedy kutoka Orijino Komedi Mpoki a.k.a Mwarabuwadubai ambapo hizi ni baadhi tu ya tweets amewahi kuziandika kwenye page yake ya twitter na unaweza kumfata pia kupitia @mwarabuwadubai
2
3
4
5
6
7
9
10
11
12
13
14
15
16

U