
Elizabeth
Mwase Programu Manager wa Mtandao wa Watoto na Vijana kutoka Imani
Mbalimbali (GNRC) akimpokea Mzee Ali Hassan Mwinyi Rais Mstaafu wa awamu
ya pili ambaye alikuwa mgeni rasmi ya Siku ya Kimataifa ya Amani
iliyoadhimishwa mwishoni mwa Juma jijini Dar es Salaam ukumbi wa Don
Bosco.
Mgeni
Rasmi Mzee Mwinyi akisalimiana na baadhi ya mabalozi na wawakilishi wa
jumuiya za maendeleo za nchi wa hisani wakati wa maadhimisho hayo jijini
Dar es Salaam.
Mgeni
Rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi akipokea
mfano wa ndege wa Amani kutoka kwa wanafunzi wa shule mbalimbali za
jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani
duniani jijini Dar.
Mgeni
Rasmi Mzee Mwinyi akihutubia wageni waalikwa (Hawapo pichani) wakati wa
sherehe za Siku ya Kimataifa ya Amani juzi asubuhi jijini Dar. Kulia ni
balozi wa Rwanda nchini Ben Rugangazi na kushoto kwa mgeni rasmi ni
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF)
Jama Gulaid.
Meza kuu.
Baadhi
ya wanafunzi wa sekondari mbalimbali za jijini ikiwamo shule ya sekondari tambaza wakitumbuiza kwa nyimbo
mbalimbali zenye ujumbe wa kudumisha Amani na upendo duniani.
Mgeni
Rasmi Mzee Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mabalozi na
wawakilishi wa ofisi za mabalozi waliohudhuria sherehe hizo kwenye
ukumbi wa Don Bosco.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hizo.
.awaasa vijana kutotumiwa na wanasiasa kwa maslahi yao
.ashangaa wajuzi walivyompachika jina la Ruksa enzi za miaka 1990s
NA SAMMSANGA BLOG
Rais
Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi amesema kuna baadhi
ya watu katika jamii hutumia elimu, ujuzi na maarifa yao kuangamiza,
kubomoa na kudumaza Ustawi wa Jamii kwa maslahi binafsi na si ya Umma. SAMMSANGA blog inaripoti.
Mzee
mwinyi amesema hayo wakati wa kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Amani
Duniani inayoadhimishwa 21th Septemba kila mwaka ambayo imefanyika
katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam, amesema kuna baadhi ya
watu wanatumia elimu yao vibaya kwa kupanga kuua watu wengine kwa
maslahi yao aidha ya kisiasa au ya kiuchumi.
“Elimu
kwa kawaida kuleta matokeo mazuri kwa jamii husika endapo itatumika
sawia kwa malengo yaliyokusudiwa na kwa maendeleo endelevu ya taifa kwa
ujumla, ila kuna baadhi ya wanajamii kutumia ujuzi huu vibaya na
kuangamiza ustawi wa jamii husika,” amesema.
Mzee
Mwinyi aliendelea kusema kwamba katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya
amani duniani yenye kauli mbiu “Education for Peace” ni lazima elimu
kwa ajili ya amani iwe endelevu hapa duniani ili iweze kuleta suluhu na
utengamano katika jamii na mataifa yote duniani.
Amesema
kwamba vijana nchini lazima waepuke kutumiwa na wanasiasa kwa maslahi
yao ya kisiasa na wajifunze kutatua matatizo yao kwa njia ya amani bila
ya kuwa na mihemko, jazba, misongo na hasira ili kuendelea kudumisha
amani na upendo katika nchi yetu ambayo ni kisiwa cha amani.
“nawaasa
vijana wakitanzania wa leo hata kama mmenyimwa haki zenu ni bora
kutumia njia ya kistaarabu na kutumia elimu mnayopata mashuleni bila
kusahau macho, masikio na vipawa vyenu mlivyopewa na mwenyezi mungu
katika kutafuta haki yenu kwa njia ya amani bila misukosuko,” aliongeza.
Mzee
Mwinyi alitumia nafasi hiyo kuwashangaa baadhi ya watu kwa kutumia
ujuzi na elimu yao kwa kumpachika jina la Ruksa bila yeye kujua
wametumia muktha gani kumpa jina hilo, lakini Mzee Mwinyi alitumia
jukwaa hilo pia kuwapa ruksa vijana kutumia elimu yao kuleta hali ya
amani na utulivu ndani ya nchi.
Kwa
upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia
watoto (UNICEF) Jama Gulaid amesema kwamba Umoja wa Mataifa uliweka
maazimio siku ya kimataifa ya amani duniani ili watu wanaogombana na
kupigana kwa shida mbalimbali kupata nafasi ya kuweka silaha zao chini
katika siku hii adhimu.
Amesema
kupitia azimio hilo ambalo lilizinduliwa mwaka 1982 kwa mara kwanza
linatambua uwepo wa watu wanaoathirika na vita katika sehemu mbalimbali
duniani na waliokwishapoteza maisha kutokana na matatizo vita vya
wenyewe kwa wenyewe.
Naye
Mratibu na Mtathimini wa Mtandao wa watoto na vijana kutoka Imani
Mbalimbali (GNRC) Bi, Joyce Mdachi amesema swala la amani na utulivu
linaanzia kwenye kaya hadi ngazi ya taifa kwahiyo ni muhimu kwa jamii na
vijana kuelewa amani inaanzia nyumbani.
“jamii
iliyolelewa katika mazingira mazuri ina nafasi kubwa ya kuleta matokeo
chanya kwenye mustakabali wa taifa kwa ujumla lakini jamii iliyolelewa
vibaya haiwezi kubadilisha taifa kwa sababu ni zao la tunda baya,”
alisema.
Mdachi
alisisitiza kwamba kuporomoka kwa maadili ndani ya jamii ya leo swala
hilo pia lilianzia kwenye kaya ya mtu mmoja mmoja hadi ngazi ya taifa
ambapo leo hii taifa linashuhudia mambo ya kifisadi, rushwa na
ubadhilifu wa mali za umma kunakofanywa na viongozi waandamizi.







No comments:
Post a Comment